Mtume صلى الله عليه
وآله وسلم amefadhilisha kinywaji cha Maziwa na kasema mtu
aombe dua ifuatayo baada ya kunywa maziwa:
((عن عبد الله بن عباس رضي الله عنهما: "من أطعمه الله
طعامًا، فليقل: اللهم بارك لنا فيه،
وأطعمنا خيرًا منه، ومن سقاه الله لبنًا فليقل: اللهم بارك لنا فيه،
وزدنا منه، فإنه ليس شيء يجزئ من الطعام والشراب غير اللبن")) رواه أحمد وأبو داودو قال الألبان
حديث حسن
((Imetoka
kwa Abdullahi Bin 'Abaas رضي الله عنهما: "Atakayelishwa chakula kutoka kwa Allaahسبحانه وتعالى aseme "Ee Mola
Mlezi Tubarikie nacho, na Utulishe (chakula) bora kuliko
hiki"; Na atakayenyeshwa Maziwa na Allaah سبحانه وتعالى
aseme, Ee Mola Mlezi Tubarikie nayo, na Tuzidishie" kwani
hakuna kitu kinachojazilia katika chakula na kinywaji isipokuwa Maziwa)) Ahmad, Abu Dawuud, na
kasema Sheikh Albaani ni
Hadithi Hassan.
No comments:
Post a Comment