- Misikiti mingi ya Mji wa Mawe ni ya ujenzi wa kawaida.
- Msikiti wa Mnara ni miongoni mwa misikiti ya zamani sana katika Mji wa Mawe. Wakati mwingine pia huitwa Msikiti wa Malindi kwa sababu upo jirani na Malindi katika Jiji la Zanzibar.
- Msikiti wa Kiislam wa Hujjatul una mojawapo ya sura za kupendeza sana kwa nje
- Msikiti wa Laghbari una mojawapo ya sura za kupendeza sana kwa ndani.
- Msikiti wa Bagh Muharmi una mnara mrefu zaidi kuliko yote.
- Msikiti wa Kizimkazi uliopo kusini ya Mji wa Mawe, ulijengwa mwaka 1107 AD na ni msikiti wa zamani sana katika kisiwa cha Unguja. Hadi leo hii bado unatumiwa na watu wa Kizimkazi .
- Hapa ni mabaki ya msikiti wa kale, Pemba (karibia mwaka 1300 AD) niliyoyapiga picha mwaka 2000 karibu na Ras Mkumbuu.
- Hizi ni picha za misikiti michache tu ya Zanzibar, ipo mingine mingi zaidi.
- Hakuna utafiti wa Misikiti ya Afrika utakaokamilika bila kutaja Msikiti mkubwa uliopo Kilwa. Wakati mwingine mwenzi, wakati mwingine mshindani wa mji wa zamani wa Zanzibar, hiki kisiwa chenye hadhi ya jiji kusini ya Zanzibar kilijenga msikiti mkubwa sana wa kale kusini ya mwa jangwa la Sahara. Mabaki mengi zaidi ya msikiti yaliyopo katika kisiwa cha Tumbatu cha Zanzibar huenda yalikuwa mojawapo ya aina hii ya ubunifu wa kupendeza.
No comments:
Post a Comment