بسم الله الرحمن الرحيم الحمد لله والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وعلى آله وصحبه أجمعين و بعد
Kauli
yako uliyosema kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ameshatakaswa na maovu na
ameshaahidiwa Pepo na kadhalika, na kwamba sisi ndio tunaohitaji kuombeana yote
hayo ni kweli kabisa. Lakini bila shaka umetatizwa kufahamu hikma ya kumswalia
Mtume صلى
الله عليه وآله وسلم hivyo In shAa Allaah سبحانه وتعالى tutakufahamisha kwa kadiri tunavyoelewa na Allaah سبحانه وتعالى Anajua zaidi.
Anasema
Allaah سبحانه
وتعالى
((إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا
الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا))
((Hakika
Allaah Anamteremshia Rehma Mtume; na Malaika Wake (wanamuombea du'aa kwa
vitendo vizuri alivyovifanya), Enyi mlioamini! Mswalieni
(Mtume - muombeeni Rehma) na muombeeni amani))[Al-Ahzaab:56] [Al-Ahzaab: 56]
Kumswalia
Mtume صلى
الله عليه وآله وسلم ni katika kumtukuza kwani
yeye ndiye Mtume wa mwisho, na hii ni neema kwetu Ummah wa Kiislamu kujaaliwa
sisi kuwa yeye ndiye Mtume wetu. Na Allaah سبحانه وتعالىAmetuambia kuwa sisi ni
Ummah bora kabisa. Bila ya yeye tusingeliweza kupata uongofu kamili (Qur-aan)
na mafunzo ya Sunnah ambayo yametutoa kizani na kutuingiza katika nuru.
Na
ikiwa Allaah سبحانه وتعالى Mwenyewe Amemtukuza kwa
kumtofautisha na Mitume mingine yote, kwani wote Amewaita kwa majina yao katika Qur-aan isipokuwa Mtume
Muhammad صلى
الله عليه وآله وسلم pekee Amemwita aidha 'Ee
Nabii', Ee Mtume. Basi sisi kumswalia ndio mojawapo ya njia ya kumtukuza.
Kwa
vile ni amri kutoka kwa Mola wetu kama
tulivyoona katika aya hiyo ya juu, na ndio maana tunamswalia mpaka kwenye
Swalah zetu za fardhi na za Sunnah, bila ya kumswalia Swalah haikamiliki.
Binaadamu
kila siku ana makosa hata awe anafanya ibada vipi, kwa hiyo ni neema kwetu
kuzidishiwa fadhila kwa kutekeleza vitendo vya Sunnah fulani ili kujiongezea
thawabu na daraja ya Pepo kwani hakuna mtu asiyependa ziada ya neema.
عنْ عبد اللَّه بن عمرو
بن العاص ، رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ
وسَلَّم يقُولُ : (( من صلَّى عليَّ صلاَةً ، صلَّى اللَّه علَيّهِ بِهَا
عشْراً)) رواهُ مسلم
Imetoka
kwa 'Abdullaah ibn 'Amru ibn Al-'Aasw رضي اللَّه عنْهُمَا kwamba kamsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلمanasema, ((Atakayeniswalia Swalah moja Allaah Atamswalia (Atampa
rahma Zake) mara kumi))[Muslim]
Maana
ya Swalah ya Allaah سبحانه وتعالى na Malaika Wake
Swalah
ya Allaah سبحانه وتعالى kwa waja Wake ni: Rahma na kuwasifu kwa Malaika.
Swalah
ya Malaika kwa Waumini ni:
Du'aa
na kuwaombea maghfirah.
Kupata
daraja ya Pepo karibu naye Mtume صلى الله عليه وآله وسلم:
عن ابن مسْعُودٍ رضي اللَّه عنْهُ أنَّ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ
عَلَيْهِ وسَلَّم قال : (( أَوْلى النَّاسِ بي يوْمَ الْقِيامةِ أَكْثَرُهُم
عَليَّ صلاةً)) رواه الترمذي وقال : حديثٌ حسنٌ
Imetoka
kwa ibn Mas'uud رضي اللَّه عنْهُ kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema, ((watu wa mwanzo kwangu (watakaokuwa karibu yangu)
siku ya Qiyaamah ni wale wanaoniswalia sana )). [At-Tirmidhy na kasema ni Hadiythi Hasan]
Vile
vile kumuombea Du'aa, mfano du'aa baada ya adhaan ni fadhila kwetu kuwa
atakayefanya hivyo atakuwa miongoni mwa atakayeombewa Shafa’ah na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم siku ya Qiyaamah.
Muumini
ni yule mwenye kumpenda khaswa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kabla ya kupenda chochote
hata nafsi yake kwani ilipoteremka Aayah hii:
((النَّبِيُّ أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنفُسِهِمْ))
((Nabii
ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao)) [Al-Ahzaab: 6]
'Umar رضي الله عنه alisema kuwa yeye anampenda Mtume kuliko chochote ila
nafsi yake. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamuambia 'Umar kuwa hadi
ampende hata kuliko nafsi yake ndipo yatakapothibitika mapenzi yake, naye 'Umar
akakubali kuwa anampenda kuliko hata nafsi yake. Kwa hiyo na sisi Waumini tuwe
na mapenzi makubwa ya kumpenda na dalili mojawapo ni kupenda kumswalia na
kufuata aliyokuja nayo na kujiepusha na aliyotukataza nayo ya uzushi (bid’ah)
na mengine.
Allaah سبحانه وتعالى Amekwishamuahidi Mtume Wake kuwa atapata malipo mengi yasiyokatika:
((وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ))
((Na kwa
hakika wewe una malipo yasiyokatika)) [Al-Qalam: 3]
Mbali
ya kuwa ni malipo yake kwa sababu ya Utume wake na kufikisha ujumbe kwa tabu na
mashaka, vile vile kumswalia kwetu kila siku katika
Swalah zetu kila mara, na kuswaliwa na Ummah mzima wa Kiislamu tokea Utume wake
hadi siku Qiyaamah ni mojawapo ya kuthibitisha kauli hiyo ya Allaah سبحانه
وتعالى.
No comments:
Post a Comment