NAFSI TATU ZENYE SIFA
TOFAUTI KABISA
Kama
Mungu Baba, Yesu na Roho Mtakatifu ni nafsi tatu zenye sifa mbali mbali kabisa
ambazo katika hizo hazishirikiani zote tatu, hapo hizo tatu haziwezi kuhesabiwa
kuwa 'Tatu katika moja' na 'Moja katika tatu'. Utatu unaweza kuunganika ukawa
umoja hasa hapo tu ambapo nafsi zote tatu zinakuwa na mienendo ile ile na sifa
zile zile na kazi zile zile na nguvu zile zile za aina moja wala hamna hata
sifa moja maalum inayoitenga moja na nafsi nyingine mbili. Hiyo inaweza kufananishwa
kiasi fulani na watoto watatu waliozaliwa kutokana na mimba moja ambao
wanafanana sana sana kabisa, hata fikra zao, maono yao na kazi za viungo vyao vinaafikiana
mno hata kwamba majaribu ya kila mmoja wao ni majaribu ya wote hao
kikamilifu bila tofauti yoyote.
Ingawaje
Yesu Kristo anatajwa mara kwa mara katika Agano Jipya akimwabudu Mungu Baba na anawasihi
wengine pia kumwabudu Yeye.
Lakini
haikuelezwa kuhusu Roho Mtakatifu akimwabudu Mungu Baba. Tena hamna kabisa
habari ya Yesu k u j a r i b u k u w a
e l e k e z a w e n g i n e k u m w a b u d u y e y e
w a l a
kumwabudu
Roho Mtakatifu sawa na taarifa ya Agano Jipya. Mtu anakanganywa na kutokutajwa
kuabudiwa kwa Yesu na Roho Mtakatifu katika Agano Jipya, lakini habari ya Mungu
Baba kuabudiwa imetajwa mara kwa mara.
Ijapokuwa
ni desturi ya kawaida ya Wakristo kumwabudu Yesu kuwa 'Mwana wa Mungu' pamoja
na kumwabudu Mungu Baba, hata hivyo hamna taarifa yoyote iliyohifadhiwa katika
maandiko ya kwamba mwana funz i
yeyot e wa Ye su Kr i s to a l iwahi kumwabudu yeye, ama Yesu
akawaelekeza kufanya hivyo katika muda wote aliokaa ardhini. Hata kama yeye
angelifanya hivyo, maswali mengi yasiyoweza kujibika yangezuka.
Ndivyo
ilivyo hali ya Roho Mtakatifu, yeye naye hakumtaka yeyote kumwabudu yeye. Kwa
nini? Ile hali imekwisha chunguzwa tayari kiasi fulani ambako hao walikuwa
'Tatu katika Moja' katika maana hii ya kwamba u t amb u z i wa o
wa k uwa p o kwa o
u l i k uwa mmo j a j u u
y a kugawanyika katika hali ama jiha tatu. Dhati ya aina hiyo haiwezi kiakili
kuhesabiwa kuwa 'watu watatu katika mmoja'. Aidha, hali ama jiha haziabudiwi,
wala hazijiabudu. Kwa kuwatambua kuwa watu watatu tofauti, wanalazimika kujijua
wanakuwapo kwa Utatukujitegemea. La sivyo, suala la kujitaja ama kuwataja
wengine kwa kusema 'Mimi', 'Wewe' na 'Yeye' halizuki asilani.
Utatu
ukitumika kwa dhati moja humaanisha sifa tu basi. Na sifa kwa kweli hazina
kikomo, haziwezi kuwa tatu tu. Tujue tusijue, Mungu anazo sifa nyingi teletele.
Kwa kumalizia mazungumzo haya, twasisitiza mara nyingine ya
kwamba
suala la wao kuabudu wao kwa wao linaweza kuzuka hapo tu ambapo hao wangekuwa
watu watatu wenye madaraka mbalimbali na sifa tofauti. Katika shauri hiyo,
mmoja tu ataabudiwa na wengine wawili wakiwa wenye daraja dogo watatazamiwa
kumwabudu yeye. Hilo
lakubaliwa, lakini ule 'Umoja katika utatu' utatoweka. Hamna njia yoyote ya
kuwa na 'Tatu katika Moja' na 'Moja katika Tatu', zote mbili hizo, wakati
huohuo mmoja. Hiyo imenikumbusha kisa kimoja cha kuchekesha ambacho ningependa
kuwaambieni. Imesimuliwa ya kwamba wakati Tamerlane alipovamia mji wa Baghdad alifurahiwa na Bwana Joha, mcheshi wa mahakama,
mpaka akaamua kumchukua pamoja naye kama
mateka na akampa kazi maalum ya kuwa mchekeshaji mkuu wa korti. Inasemekana
safari moja Joha aka j awa na shauku ya
kul a nyama akiwa
peke yake bi l a kushirikiana na wengine. Akashikwa na
kiherehere hicho sana
hadi hakuweza kujizuia. Basi akanunua nyama kilo mbili nzuri kabisa kutoka kwa
muuza nyama. Alipomkabidhi mkewe nyama hiyo akaagiza kuichoma vizuri sana , lakini akamuambia
hakuna atakayeila isipokuwa yeye peke yake, yaani Joha, hata mkewe hawezi
kuionja. Sasa kwa bahati mbaya, mkewe alipokwisha tu kuichoma vizuri sana nyama hiyo, ghafula
wakaja nduguze kadha kumtembelea. Hiyo ilikuwa furaha aliyopata ghafula, lakini
ikawa habari mbaya ya kwa Joha.
Harufu
nzuri ya kuvutia iliwashinda hao ndugu za mkewe, na matokeo ndiyo unaweza
kukisia. Wakala na kumaliza mpaka
kipande cha mwisho kisha wakamwaga dada yao
ambaye sasa akaanza kuhangaika. Lakini akajituliza kabla h a j a w a s i l
i n y u m b a n i B w a n a
J o h a , m a a n a Ukristo -
Safari kutoka Hakika
kuelekea kwenye Ubunifualishawaza
hila ama udhuru fulani ili kujiokoa katika hali hiyo ngumu. Joha alipoingia na
akasikia harufu nzuri ya kuvutia ya nyama iliyochomwa ambayo ilikwisha liwa
tayari, akamwagiza mkewe kuleta haraka hiyo nyama.
Hapo
mkewe akiashiria kwenye paka wa Joha aliyekuwa amemfuga kwa shauku sana , akasema:
Toa
nyama yako kutoka katika paka huyu, ukiweza.
Maana
nilipokuwa nimeshughulika, huyu akaila yote. Hapo haraka sana Joha akamshika paka na kumpima katika
mizani. Kumbe uzito wake ulikuwa kilo mbili barabara. Basi kamwelekea mkewe kwa
upole na akamuuliza: Mke wangu mpenzi, hakika nimekubali ulivyosema, lakini
kama hiyo ndiyo nyama yangu, basi yuko wapi paka wangu; na kama
huyu ndiye paka wangu, basi nyama yangu iko wapi!
Achilia
mbali vichekesho, nisingependa kujadili suala hilo juu ya msingi wa mafunzo halisi na ya
kweli ya Yesu. Maandiko haya shabaha yake hasa ni kuchunguza itikadi za sasa
hivi za Kikristo ambazo twaamini kwamba zimepotoka na kwenda mbali kabisa na
mafunzo ya asili ya Yesu. Tukiisha kanusha habari ya Yesu kuabudiwa ndani ya
Biblia, inatulazimu kufafanua sehemu ya pekee ndani ya Biblia, yaani Luka 24:52
ambamo Yesu anaonekana aliabudiwa. Wengine wanasema ya kuwa mstari huo unatoa
ushahidi ya kwamba Yesu aliwahimiza kumwabudu. Wataalamu wa Kikristo wa zama
hizi wanaelewa sana ya kwamba mistari hiyo
imekwisha hakikishwa kuwa ya uwongo iliyoongezwa baadaye wala hakuna haki ya kuihesabu
mistari hiyo kuwa sehemu halisi ya Injili ya Mt. Luka .
Hebu sasa tugeukie kwa suala la desturi ya kawaida kwamba je hiyo inathibitika
kwa ushuhuda uliomo katika Injili ama hapana. Sawa na desturi ya kawaida, Yesu
anaabudiwa akiwa 'Mwana wa Mungu' katika madhehebu mengi ya Kikristo.
Hata
hivyo wote hao wanakiri ya kwamba Yesu huyohuyo mwenyewe alikuwa
anamwabudu
Mungu Baba peke yake. Bure kabisa nimewauliza mara nyingi wataalamu wa Kikristo
wenye ujuzi mwingi ya kwamba kwa nini Yesu alimwabudu UtatuMungu Baba ikiwa
yeye mwenyewe alikuwa sehemu ya Mungu isiyoweza kutenguka na alikuwa
ameunganika naye kabisa kikamilifu kwa kuleta maana ya umoja japo nafsi tatu
zilikuwepo? Je siku yoyote aliwahi kumwabudu Roho Mtakatifu pia aliye nafsi ya
tatu katika Utatu? Je, alijiabudu wakati wowote? Je, Roho Mtakatifu alimwabudu
Yesu siku yoyote? Na je, Baba aliwahi siku yoyote kumwabudu yeyote miongoni mwa
wawili wengine wa Utatu? Kama hapana kwa nini? Pengine majibu ya suala hilo yatawalazimisha
Wakristo kukiri ya kwamba Baba anacho cheo kikubwa zaidi kuliko nafsi mbili
nyingine za Utatu.
Inathibitika
kutokana na hiyo ya kwamba sehemu tatu za Utatu haziko sawa katika daraja.
Hivyo, hao ndio 'Watatu katika Watatu' kama
kwa vyovyote wako watatu, lakini siyo kabisa 'Watatu katika Mmoja'. Wakati
mwingine wataalamu wa Kikristo wanapokabiliwa na swali la Yesu, wanayemwamini kuwa Mwana wa Mungu, k
u m w a b u d u M u n g u B a b a ,
h u s e m a Y e s u - m t u n d i y e aliyemwabudu Mungu Baba, siye Yesu
Mwana aliyemwabudu Yeye. Hiyo inatupeleka nyuma tena kwenye mazungumzo tuliyokwisha
fafanua tayari. Je, mwili huohuo mmoja wa Yesu ulikaliwa na nafsi mbili, moja
yenye dhamira ya binadamu na nyingine ya Mwana wa Mungu?
Aidha,
kwa nini mtu ndani ya Yesu aliepa na kumpuzilia mbali kabisa Mwana wa Mungu
aliyekuwemo ndani yake asimwabudu Kr i s to ha t a ma r a
moj a ? Huyo huyo Ye su-mtu a l i t akiwa kumwabudu Roho Mtakatifu pia
aliye nafsi ya tatu katika Utatu, lakini mbona hakufanya hivyo katu! Ibada ni
tendo la moyo na roho ambalo pengine huoneshwa kwa alama za kimwili, lakini
lina mizizi yake katika fahamu na maono ya dhamiri ya mtu. Hivyo inapaswa kungunduliwa nani aliabudu pindi Yesu Kristo
alipomwabudu Mungu. Tumekwisha eleza
jambo
hilo hapo kabla pamoja na matatizo yake ya kwamba Kr i s to, Mwana
wa Mungu, ndiye
a l iyemwabudu Mungu.
Kinyume
chake, kama alikuwa ni mtu aliyemwabudu Mungu Baba, na huyo mtu hakumwabudu
Kristo, kwa nini basi Wakristo Ukristo - Safari
kutoka Hakika kuelekea
kwenye ubunifuwanaukaidi mfano huo bora wa Yesu mwenyewe? Kwa nini wanaanza
kumwabudu Kristo pamoja na Mungu, ilhali Yesu-mtu hakumwabudu mwenzake Kristo
japo alikaa karibu yake mno.
NAFSI TATU ZENYE SIFA
ZIFANANAZO ZILIZO SAWA:
Hebu
tuchunguze mara nyingine tena, lakini safari hii kwa jiha tofauti kabisa,
kanuni ya 'Tatu katika Moja' ndani ya Utatu, tukizichukua kuwa dhati tatu
tofauti lakini zenye sifa zilezile zifananazo kabisa kikamilifu. Hapa
hatuzungumzii dhati moja yenye sifa mbalimbali zilizounganika pamoja, bali
twazungumzia dhati tatu kama watoto watatu
waliozaliwa katika mimba moja.
Twazungumzia
hao watatu ambao wanafanana wao kwa wao sana kabisa
hata kwamba kufanana kwao hakuishii tu katika kufanana umbo na sura, bali hata
fikara zao na maono yao
pia ni ya aina moja. Wanashirikiana katika fikira zao, maono yao
na majaribu yao
kwa namna moja kabisa. Hapo mtu hana budi kukiri ya kwamba nafsi mbili katika
utatu hazina kazi tena, ni bure kabisa. Kama
hizo mbili zikiondolewa mbali, hazitaleta kasoro yoyote
ile
iwayo kwa nafsi iliyobaki ya Utatu ambayo nafsi hiyo itakuwa kamilifu peke
yake.
Quran Tukufu pia inauliza swali hilo inapodokeza ya
kwamba kama Mungu akiamua kumuangamiza na
kumfutilia mbali kabisa Yesu Kristo na Roho Mtakatifu, tofauti gani itatokea
kwa utukufu wake, Umilele wake na Ukamilifu wake, na ni nani awezaye kumzuia
Yeye asifanye hivyo (5:18). Hiyo inamaanisha ya kwamba sifa zote za Mungu
zitaendelea kufanya kazi milele na kwa hivyo itikadi ya Utatu ilivyoelezwa hivi
sasa haina maana wala haihitajiki Utatu
Lakini
kama ifikiriwe ya kwamba dhati tatu hizo za utatu zinafanya kazi mbalimbali,
hapo bila shaka sehemu zote tatu za utatu zitahitajika ili kufanyiza Mungu.
Hata hivyo hapo patakuwa na Miungu watatu tofauti wanaosaidiana wao kwa wao na
kukaa pamoja kwa amani kamilifu na hapo wanaweza kuhesabiwa 'Miungu Watatu
katika Watatu' wala hapana 'Miungu Watatu katika Mmoja'. Na kama isemwe ya kuwa
Utatu ndiyo kama mtu mmoja mwenye viungo
mbalimbali vinavyofanya kazi tofauti vikiunganika ndani ya mtu mmoja, hapo bila
shaka Umoja utakuwepo lakini Utatu utatoweka. Lakini tukumbuke ya kwamba
hatuzungumzii hapa
mtu
mmoja mwenye viungo kadha vinavyofanya kazi, bali watu watatu wanaofanana
kabisa kwa kila hali na kila jiha, na kila mmoja akifanya kazi hizohizo za aina
moja na hata hivyo kila moja anabaki kuwa mtu binafsi peke yake. Iliyojadiliwa
ni hali ya mtu mmoja mwenye viungo kadha. Mpaka hapo sawa, hamna kilicho
kinyume cha akili.
Lakini
viungo vikihesabiwa kuwa watu na palepale watu hao wote wakiwa pamoja
wanafanyiza mtu mmoja kwa jumla, hapo habari hiyo inakuwa kinyume cha akili wala
haiwezi kukubalika. Ni sawa kuwa kila kiungo kina kuwapo kwake, lakini kuwapo
huko ndiyo sehemu tu ya mtu ambaye si tu kwamba anacho kiungo hicho tu kimoja
bali anavyo viungo vingine pia. Viungo hivyo vikiwa pamoja ndani ya mtu huitwa 'mtu'
kwa jumla. Naam, baadhi ya viungo vinafanya kazi ya muhimu zaidi na vingine
vina kazi si ya muhimu sana ,
na mtu anabaki kuwa mtu bila ya viungo hivyo vyenye kazi isiyo muhimu, lakini
mtu huyo atakuwa si mkamilifu, bali atakuwa na kasoro fulani. Mtu mkamilifu
hupaswa kuwa na viungo vyote vile anavyokuwa navyo mtu yeyote kikawaida, na
jumla ya viungo hivyo hufanyiza mtu mkamilifu.
Tukichukua
mfano wa mtu mmoja aitwaye Paulo, mtu hawezi kusema ya kwamba kwa kuwa ini,
moyo, mapafu na mafigo ya Paulo ni vitu maalum mbalimbali ambavyo vina kazi
mbalimbali, Ukristo - Safari kutoka Hakika
kuelekea kwenye Ubunifubasi kwa
hiyo hivyo ni nafsi mbalimbali zilizokamilika ambazo kila nafsi katika hizo ni
sawasawa na Paulo. Kila kiungo chaweza kuwa Paulo hapo tu ambapo kwa mfano
mafigo peke yake yafanye kazi zote kwa jumla anazofanya Paulo, na kadhalika
kila kiungo kiwe hivyo hivyo. Jambo hilo
linamaanisha ya kwamba viungo hivyo vikikosekana, hakuna badiliko litakalotokea
katika Paulo. Au tuseme kwamba Paulo bado atabaki kuwa Paulo kikamilifu kama viungo vyake yaani mapafu, moyo, mafigo na ubongo,
kwa hakika viungo vyote vikiondolewa mbali. Hiyo ni kwa sababu katika ukaguzi
wa mwisho viungo hivyo vyote vinafanana, na dhati ya Paulo inabakia tu pale
pasipo kujali viungo hivyo vipo ama havipo.
No comments:
Post a Comment